Rais wa China atoa hotuba ya kimaandishi baada ya kuwasili katika Marekani

(CRI Online) Septemba 24, 2026

Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba ya kimaandishi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Joint Base Andrews ulioko jimboni Maryland nchini Marekani.

Kwenye hotuba yake rais Xi amesema, China na Marekani zote ni nchi kubwa kiuchumi, na kwa muda mrefu, watu wa China na Marekani wamekuwa na mawasiliano ya kirafiki, huku maslahi za pande mbili zikiungana kwa kina. Amesema nchi mbili zinatakiwa kuwa washirika badala ya wapinzani, na dira ya China ya kutimiza ustawishaji mkubwa wa taifa na ajenda ya Marekani ya kuifanya nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi (MAGA), vinaweza kwenda sambamba na kukamilishana, jambo ambalo litanufaisha dunia nzima.

Pia amesema, wakati rais wa Marekani Donald Trump alipofanya ziara nchini China mwezi wa Mei mwaka huu, walikubaliana kuunda uhusiano tulivu wa kiujenzi na kimkakati kati ya China na Marekani, ili kutoa mwongozo wa kimkakati kwa ukuaji wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika siku za baadaye. Pande mbili za China na Marekani zinatakiwa kusonga mbele kwa pamoja, kuhimiza kuundwa kwa uhusiano imara unaoangazia ushirikiano, na wenye ushindani unaofaa, tofauti zinazodhibitiwa, na amani inayotarajiwa, na kufuatanjiasahihi ya China na Marekani kuishi pamoja kwa amani katika zama mpya. Rais Xi ameeleza imani yake na jambo hilo.

Rais Xi amesema, anatarajia kufanya mawasiliano ya kina na rais Trump juu ya masuala makubwa yanayohusiana na uhusiano kati ya nchi mbili na hali ya dunia, kuzidi kuongeza maana ya uhusiano imara wa kiujenzi na kimkakati kati ya China na Marekani, na kupanua nafasi ya ushirikiano na mawasiliano katika nyanja mbalimbali kati ya China na Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha