Lugha Nyingine
Meli ya matibabu ya Jeshi la China yakamilisha jukumu la matibabu nchini Mauritania
Meli ya matibabu ya Jeshi la Majini la China imeondoka nchini Mauritania jana Jumanne baada ya kukamilisha jukumu la afya na matibabu katika ziara ya kirafiki ya siku saba nchini humo.
Meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Urafiki ya Nouakchott saa nne asubuhi kwa saa za huko, na kuagwa na maofisa wa jeshi na serikali ya Mauritania, maofisa kutoka Ubalozi wa China nchini humo, wakazi wa huko na wawakilishi wa jamii na kampuni za Wachina nchini humo.
Tangu kuwasili nchini Mauritania Septemba 15 kama kituo cha kwanza cha Jukumu la Amani 2026, wafanyakazi wa afya katika meli hiyo wamepokea wagonjwa 6,864, kufanya pasuaji 38, ikiwemo upasuaji wa mifupa, upasuaji wa magonjwa ya kawaida, na upasuaji wa macho, na kufanya kaguzi 143 za afya ya mwili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



