Lugha Nyingine
Idadi ya faru weusi nchini Tanzania yaongezeka zaidi ya maradufu katika muongo mmoja
Ofisi ya Tanzania ya Mfuko wa Wanayamapori Duniani (WWF) imesema Idadi ya faru weusi nchini humo imeongezeka zaidi ya maradufu katika muongo uliopita, jambo linaloashiria maendeleo katika juhudi za uhifadhi wa wanyamapori.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika WWF nchini Tanzania, Joan Itanisa amesema kuongezeka huko kunaonyesha matokeo ya juhudi za miaka mingi zilizofanywa na serikali, washirika wa uhifadhi na jamii katika kulinda wanyamapori na kuishi pamoja kwa amani kati ya binadamu na wanyamapori.
Hata hivyo, shirika hilo limeonya kuwa kupotea na kugawanyika kwa makazi ya wanyama kunakosababishwa na upanuzi wa kilimo, malisho ya mifugo na ujenzi wa makazi, pamoja na mabadiliko ya tabianchi, migogoro kati ya binadamu na wanyamapori, na matumizi yasiyo endelevu ya maliasili vinaendelea kutishia wanyamapori.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



