Lugha Nyingine
Rwanda na Ubelgiji zarudisha uhusiano wa kibalozi
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Rwanda imetoa taarifa ikisema, Rwanda na Ubelgiji Jumanne ziliamua kwa pamoja kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati yao.
Taarifa ya pamoja kuhusu uamuzi huo ilitolewa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Rwanda Bw. Olivier Nduhungirehe, na naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje, mambo ya Ulaya na ushirikiano wa maendeleo wa Ubelgiji Maxime Prevot.
Taarifa imesema uamuzi huo unafuatia mfululizo wa mikutano na mawasiliano yasiyo rasmi yaliyofanyika kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na Ubelgiji katika miezi ya hivi karibuni iliyopita, ambapo nchi mbili zimeishukuru Qatar kwa kuwezesha mkutano wa kwanza kati ya mawaziri hao huko Doha Juni 2025. Taarifa pia imesema nchi hizo mbili zitafungua tena ubalozi wa kila upande katika upande mwingine katika siku za usoni.
"Ubelgiji na Rwanda zimesisitiza kujitolea kwao kudumisha mazungumzo yaliyo ya wazi na udhati, na pande mbili zimefikia maoni kwa kauli moja kuhusu kanuni mpya kama vile kutoingilia mambo ya ndani, kuheshimiana, na kufanya mawasiliano ya kiujenzi, kanuni ambazo zitaongoza uhusiano wa baadaye wa pande mbili."
Tarehe 17 Machi 2025, Rwanda ilikatisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Ubelgiji, ikiishutumu kwa kuiharibu Rwanda "kabla na wakati wa mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Ubelgiji ilionekana kuwa mhusika mkubwa mwenye mabavu wa kupinga Rwanda katika historia."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



