Lugha Nyingine
Maonyesho ya Usafiri wa Anga na Ulinzi ya Afrika yafanyika Afrika Kusini
Hivi karibuni, Maonyeshoya ya 13 ya Usafiri wa Anga na Ulinzi ya Afrika yalifanyika katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Waterkloof kilichoko mjini Centurion, karibu na mji mkuu Pretoria, nchini Afrika Kusini.
Maonyesho hayo yakiwa na kauli mbiu ya “Dirisha la kuelekea Afrika na kuhudumia ushirikiano katika nyanja za ulinzi na usafiri wa anga,” yameshirikisha zaidi ya makampuni 250 kutoka nchi 33 za Afrika, Asia, Ulaya na Amerika, ambapo uvumbuzi wa sekta ya ulinzi katika akili bandia, mifumo ya kujiendesha na usalama wa mtandao umefuatiliwa zaidi.
Shirika la Viwanda vya Anga la China (AVIC) lilishiriki kwenye maonyesho hayo na kuonyesha aina mbalimbali za vifaa vya usafiri wa anga, zikiwemo ndege za kivita J-10 CE na JF-17 “Thunder”, na ndege kubwa ya usafirishaji Y-20, kwa lengo la kuimarisha mawasiliano ya kimataifa ya ulinzi na kupanua fursa za ushirikiano wa kunufaishana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



