Lugha Nyingine
Uongozi wa CPC wajadili masuala muhimu kuhusu utawala wa ndani wa Chama na kupanga tarehe za mkutano mkuu wa Kamati Kuu
Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Xi Jinping, Jumatatu aliongoza mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC. Mkutano huo ulijadili masuala muhimu kuhusu kuimarisha utawala wa ndani wa Chama kwa ukamilifu na kina na kwa msimamo thabiti, na kupanga tarehe za mkutano mkuu wa Kamati Kuu utakaofanyika mwezi Oktoba.
Mkutano huo umeamua kuwa mkutano wa tano wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC uitafanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Oktoba mjini Beijing. Pia, uliamua kuwasilisha waraka kwenye mkutano mkuu, ambao unahusu uamuzi wa Kamati Kuu ya CPC wa kuimarisha utawala wa ndani wa Chama kwa ukamilifu na kina na kwa msimamo thabiti, ili kujadiliwa.
Rasimu ya awali ya uamuzi huo ilisambazwa kwa wanachama wa CPC na wasio wanachama ili kupata maoni yao, na ilipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wale walioshirikishwa.
Mkutano huo ulibainisha kuwa waraka huo unatoa tathmini ya kweli kuhusu mafanikio na uzoefu katika kuendeleza utawala wa ndani wa Chama, unatoa uchambuzi wa kina wa hali na majukumu yanayokabili ujenzi wa Chama kwa sasa na katika kipindi kijacho, na unaweka mipango ya kimkakati ya kuendeleza zaidi utawala wa ndani wa Chama kwa ukamilifu na kina na kwa msimamo thabiti.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



