Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China kufanya ziara rasmi nchini Marekani kuanzia tarehe 23 hadi 25 Septemba
(CRI Online) Septemba 22, 2026
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun ametangaza kuwa rais Xi Jinping wa China atafanya ziara rasmi nchini Marekani kuanzia tarehe 23 hadi 25 mwezi Septemba kwa mwaliko wa Rais Donald Trump wa Marekani.
Akiongea na wanahabari Bw. Guo amesema wakati wa ziara hiyo, rais Xi na rais Trump watafanya mazungumzo ya kina kuhusu masuala muhimu yanayohusu uhusiano kati ya China na Marekani pamoja na amani na maendeleo ya dunia.
Ameongeza kuwa China iko tayari kushirikiana na Marekani kuongeza maudhui ya uhusiano wa kiujenzi wenye utulivu wa kimkakati, kuimarisha mazungumzo na ushirikiano, kushughulikia ipasavyo tofauti zilizopo, na kuendelea kuchangia ustawi wa watu wa pande zote mbili pamoja na amani, utulivu na maendeleo ya dunia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



