Ushirikiano kati ya China na Afrika katika elimu ya ufundi wa kazi waleta ujuzi, na kufungua fursa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 21, 2026

Tola Tsegaye Alemu (Kulia) kutoka Ethiopia akiendesha roboti ya viwandani chini ya mwongozo wa  mwalimu katika Chuo Kikuu cha Teknolojia na Elimu cha Tianjin kaskazini mwa China. Tianjin, Juni 27, 2024. (Xinhua/Sun Fanyue)

Kwenye karakana moja mjini Ongwediva, kaskazini mwa Namibia, vipande vya kitambaa vinapimwa, kukatwa, na kushonwa na Wilhemina Amadhila. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye atapeleka ufundi huo kwenye Mashindano ya 48 la Ujuzi Duniani yatakayofanyika Septemba 22-27 mjini Shanghai, China, alisema: "Kila mshono huunganishwa ili kuunda vazi la kuvutia."

Bi. Amadhila na vijana wengine 16 wa Namibia watashindana katika vipengele tofauti vya mashindano hayo. Mbali na Namibia, nchi nyingine za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Misri, Afrika Kusini, na Morocco pia zinashiriki kwenye mashindano hayo kuonyesha ufundi na ujuzi wao wa kitaaluma wa kazi mbalimbali.

Hii si mara ya kwanza kwa washindani wa Afrika kushiriki katika mashindano ya ufundi stadi wa kazi nchini China. Ushiriki wao kikamili unatoa mwanga wa kukua kwa ushirikiano kati ya China na Afrika katika elimu ya ufundi wa kazi, jambo ambalo limesaidia kuwapa waafrika wengi ujuzi na fursa ya kupata uzoefu wa kivitendo.

Kwenye mashindano ya Ujuzi wa Vyuo vya Ufundi wa kazi Duniani ya 2025 yaliyofanyika mjini Tianjin, China, mwanafunzi wa Angola Massak Ventura Noquena Eduardo alipata medali ya fedha kutokana na ujuzi aliopata kuhusu roboti za viwandani na mnyororo wa uzalishaji otomatiki aliojifunza kutoka kwa walimu wa China. Alisema "Natumai kutumia nilichojifunza katika ukuaji wa viwanda wa Angola."

Picha hii iliyopigwa Novemba 14, 2025, inaonesha  hali ya fainali kwenye Mashindano ya Ujuzi wa Vyuo vya Ufundi kazi Duniani mjini Tianjin, kaskazini mwa China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

Picha hii iliyopigwa Novemba 14, 2025, inaonesha hali ya fainali kwenye Mashindano ya Ujuzi wa Vyuo vya Ufundi kazi Duniani mjini Tianjin, kaskazini mwa China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha