Migodi mitano yaporomoka mashariki mwa Sudan

(CRI Online) Septemba 21, 2026

Migodi mitano iliyoko eneo la Oni katika jimbo la Bahari Nyekundu, mashariki mwa Sudan iliporomoka tarehe 19, na kusababisha vifo vya watu kumi na wengine 21 kujeruhiwa, huku wengine wakikwama ndani ya migodi.

Mashuhuda wamesema kazi ya uokoaji bado inaendelea, na idadi ya watu wasiojulikana walipo bado haijathibitishwa. Baadhi ya majeruhi wamepelekwa Bandari ya Sudan iliyoko umbali wa takriban kilomita 300 kutoka kwenye migodi.

Asasi ya kiraia ya Sudan “Shirika la Dharura la Dar Hamar” na Kampuni ya Maliasili ya Madini ya Sudan wametoa taarifa wakithibitisha kutokea kwa ajali hiyo. “Shirika la Dharura la Dar Hamar” limesema hadi sasa miili 10 imepatikana, na majeruhi 21 wameokolewa. Kampuni ya Maliasili ya Madini ya Sudan haikutangaza idadi ya vifo na majeruhi kwenye taarifa yake.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha