Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na Rubio kwa njia ya simu kuhusu maingiliano ya ngazi ya juu

(CRI Online) Septemba 18, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana alifanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Marco Rubio kwa njia ya simu kuhusu maingiliano ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili.

Wakati wa mazungumzo yao, Bw. Wang alibainisha kuwa diplomasia ya wakuu wanchi ndiyo nguzo ya uhusiano kati ya China na Marekani, akisemapande hizo mbili zinapaswa kujiandaa kwa hatua inayofuata ya mazungumzoya ngazi ya juu kwa kuzingatia usawa, heshima na manufaa ya pande zote, kuimarisha mawasiliano, kuendeleza ushirikiano, kudhibiti tofauti, kuheshimu maslahi makuu ya upande mwingine, na kutoa ujumbe chanya kwamba nchi hizo mbili zimejitolea kuendeleza uhusiano wao wa kiujenzi na wenye utulivu wa kimkakati, pamoja na kuhimiza kwa pamoja amani na maendeleo duniani.

Aidha, Bw. Wang amebadilishana mawazo na Bw. Rubio kuhusu hali ya Mashariki ya Kati na masuala mengine.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha