Lugha Nyingine
China yaendelea kuwa nchi mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa EAC
China imeendelea kuwa nchi mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika robo ya pili (Q2) ya 2026, wakati thamani ya jumla ya biashara zake na eneo hilo ikikua kwa asilimia 37 ikilinganishwa na mwaka jana na kufikia dola bilioni 52.3.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Takwimu za Kila Robo ya EAC iliyotolewa Jumatano wiki hii, mauzo ya nje ya EAC kwa China yaliongezeka karibu maradufu kutoka dola za kimarekani bilioni 5.7 za robo ya pili ya mwaka 2025 hadi dola za kimarekani bilioni 10.7 mwaka 2026 kwa kipindi hiki, yakichangiwa kwa kiasi kikubwa na bidhaa za madini na malighafi nyingine.
Huku uagizaji kutoka China pia umeongezeka hadi dola bilioni 7.1 kutoka dola bilioni 4.7 za mwaka jana. Kwa ujumla, mauzo ya nje ya EAC yaliongezeka kwa asilimia 41.3 na kufikia dola bilioni 26.3, huku uagizaji ukiongezeka kwa asilimia 32.9 na kufikia dola bilioni 26.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



