Lugha Nyingine
Ugonjwa wa kipindupindu waendelea kuenea mashariki mwa DRC wakati nchi hiyo inapambana na Ebola
Ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kuenea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku vituo vya matibabu huko Bukavu, mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kusini vikishuhudia ongezeko la wagonjwa, wakati ambapo nchi hiyo inapambana na mlipuko wa Ebola.
Mwuguzi mkuu wa kituo cha matibabu ya kipindupindu katika Hospitali ya Saint Mathieu mjini Bukavu, amesema wagonjwa wapya wanaendelea kuwasili siku nzima, wengi wao wakiwa katika hali mbaya.
Wakati ufuatiliaji wa kitaifa na kimataifa umeangazia mlipuko unaoendelea wa homa ya Ebola, ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kuenea katika jamii huko Bukavu na katika mkoa wa Kivu Kusini, hali inayoongeza shinikizo kwa mfumo wa afya ambao unakabiliwa na dharura mbalimbali.
Kwa mujibu wa Shirika la Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA), kati ya Januari na Agosti mwaka huu, DRC imerekodi wagonjwa zaidi ya 39,400 wanaoshukiwa kuwa na kipindupindu pamoja na vifo 1,173, na mikoa ya mashariki ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini ikiwa kiini cha mlipuko huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



