Lugha Nyingine
Meli ya hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Mauritania kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu.

Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini la China, inayoitwa "Meli ya Baraka" inatia nanga katika Bandari ya Urafiki huko Nouakchott, Mauritania, tarehe 15 Septemba 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)
Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini la China, inayoitwa "Meli ya Baraka (Auspicious Ark)" iliwasili Jumanne nchini Mauritania kwa ziara ya kirafiki ya siku saba, ambapo itatoa huduma za matibabu. Meli hiyo ya hospitali, ambayo inatekeleza "Jukumu la Masikilizano 2026" ilitia nanga saa nne asubuhi katika Bandari ya Urafiki mjini Nouakchott.
Maofisa wa jeshi na serikali ya Mauritania, wanajeshi, balozi wa China nchini Mauritania, wafanyakazi wa ubalozi wa China, wajumbe wa jumuiya ya Wachina na makampuni ya China, pamoja na wakazi wa huko, walishiriki kwenye hafla ya mapokezi bandarini.
Katika kipindi cha ziara hiyo, meli hiyo ya hospitali itatoa huduma za matibabu ndani ya meli yenyewe, huku madaktari wakitembelea vituo vya afya vya eneo hilo na vikosi vya jeshi la Mauritania ili kutoa ushauri wa kitaalamu, kutoa mafunzo ya kimatibabu na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu.
Kwenye majukumu hayo pia watafanya tafrija ya mapokezi ndani ya meli, pamoja na shughuli za kitamaduni na kubadilishana uzoefu kati ya wafanyakazi wa nchi hizo mbili.
Mauritania ni kituo cha kwanza cha "Jukumu la Masikilizano 2026." Hii ni ziara ya pili kufanywa na meli ya hospitali ya jeshi la majini la China nchini humo.

Picha hii inaonyesha meli ya hospitali ya kikosi cha majini la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, inayoitwa "Meli ya Baraka (Auspicious Ark)", katika Bandari ya Urafiki huko Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, tarehe 15 Septemba 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Meli ya hospitali ya kikosi cha majini la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, inayoitwa “Meli ya Baraka (Auspicious Ark)”, inakaribishwa na bendi ya Mauritania baada ya kufika kwenye Bandari ya Urafiki huko Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, tarehe 15 Septemba 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Picha iliyopigwa kutoka angani inaonyesha meli ya hospitali ya kikosi cha majini la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, inayoitwa “Meli ya Baraka (Auspicious Ark)” katika Bandari ya Urafiki mjini Nouakchott, Mauritania, tarehe 15 Septemba 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



