Lugha Nyingine
China yazihimiza Iran na Marekani kurejea kwenye Makubaliano ya Maelewano ya Islamabad
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi Jumatano alifanya mazungumzo na mwenzake wa Iran Seyyed Abbas Araghchimjini Beijing.
Wang amesema kuendelea kwa mapambano kati ya Marekani na Iran hakuendanina maslahi ya pamoja ya pande husika na jumuiya ya kimataifa. China inazihimiza Iran na Marekani zijizuie, kurejea kwenye Makubaliano ya Maelewano ya Islamabad haraka iwezekanavyo, kujenga upya mfumo wa mazungumzo chini ya msingi wa makubaliano yaliyofikiwa, na kufanya mazungumzo halisi juu ya masuala yanayofuatiliwa.
Kwa upande wake, Bw. Araghchi amesema Iran haitaki mapambano yaendelee, na kutaka kutafuta ufumbuzi kupitia njia ya kidiplomasia, na kulinda kithabiti haki na maslahi yake. Aidha ameeleza kuwa Iran inaona kuwa Makubaliano ya Maelewano kati ya Marekani na Iran bado yanafanya kazi, na imefikia mpango na Oman juu ya kufungua upya Mlango bahari wa Hormuz, akiongeza kuwa nchi hiyo inaihimiza Marekani itimize ahadi zake kwa dhati.

people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



