Lugha Nyingine
Kiongozi wa mkoa wa Hong Kong asema kipindi cha 2026-2030 ni muhimu kwa Hong Kong kutumia fursa za maendeleo

(Picha/Xinhua)
Kiongozi Mkuu wa mkoa wa Utawala maalum wa Hong Kong, China (HKSAR) Bw. John Lee, amesema kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) ni kwa Hong Kong kutumia fursa ya kuharakisha mabadiliko kutoka hali ya utulivu hadi ustawi, kuboresha hali ya maisha ya jamii, na kujenga makazi bora kwa wote.
Akiwasilisha mpango wa kwanza wa miaka mitano wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wa Hong Kong (2026-2030), Bw. Lee amesema kipindi hiki kinatoa fursa za kimkakati kwa Hong Kong kukumbatia kikamilifu mienendo ya kisasa, kuimarisha na kuboresha uwezo wake wa ushindani, kuhimiza vichocheo vipya vya ukuaji, na kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii yenye ubora wa juu. Amesema "hii ni miaka mitano yenye matumaini kwetu kujumuika na kuchangia katika maendeleo ya taifa kwa ujumla."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



