Lugha Nyingine
Benki ya AfDB yahimiza mageuzi muhimu kujenga mifumo imara ya chakula ya Afrika
Ofisa mwandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB amesema katika kongamano la mtandaoni, kuwa mageuzi ya sera na fedha yanayolengwa ni muhimu kulinda mifumo ya chakula ya Afrika kutokana vizuizi vya kimataifa vinavyoongezeka.
Ofisa katika ofisi ya naibu mkuu wa benki hiyo anayeshughulikia kilimo, na maendeleo ya binadamu na jamii Bw. Martin Fregene, amesema mshtuko wa nje ikiwemo milipuko ya magonjwa, migogoro na mivutano ya siasa za kijiografia, vimeathiri vibaya utoaji wa chakula barani Afrika.
Ili kujenga ustahimilivu wa muda mrefu, Bw. Fregene amehimiza nchi za Afrika kuweka kipaumbele katika ufadhili wa ndani, kasi kwenye matumizi ya teknolojia, mipango ya tabianchi inayoongozwa na jamii, na maunganisho imara zaidi ya soko.
Ameongeza kuwa mifumo ya chakula siku zote inaathiriwa na mishtuko ya kimataifa, ikiwemo janga la COVID-19 na mapigano yanayovuruga ugavi wa mbolea na pembejeo nyingine za kilimo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



