Lugha Nyingine
Uagizaji wa pikipiki na bajaji za umeme kutoka China waongezeka huku uwekezaji wa vyombo vya usafiri vya umeme barani Afrika ukiwa mbalimbali
Uagizaji wa pikipiki na bajaji za umeme kutoka China uliongezeka sana barani Afrika katika nusu ya kwanza ya 2026, ongezeko linaloonesha uanuai katika mpito wa bara hilo kuelekea kutumia vyombo vya usafiri vya umeme.
Pikipiki na bajaji zinachangia sehemu kubwa ya vyombo vya usafiri kwenye barabara za Afrika na zinatumika zaidi kibiashara. Kwa hivyo, kubadili matumizi ya injini za petroli na dizeli na kuingia kwenye umeme kunaweza kupunguza matumizi ya mafuta na uchafuzi wa hewa mijini.
Nchi za Kaskazini mwa Afrika kama Morocco, Misri na Algeria ziliongoza kwa ongezeko la 60% la uagizaji barani humo, hadi dola milioni 114.6. Eneo hilo limekuwa kivutio kikubwa cha pikipiki za umeme za China zilizotengezwa kikamilifu.
Wakati huo huo, uwekezaji katika makampuni mapya ya magari ya umeme umejikita katika Afrika Mashariki na Kati, ambapo makampuni yanajenga viwanda vya kuunganisha vya ndani, mitandao ya kubadilishana betri na mifumo ya ikolojia ya pikipiki za kibiashara.

people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



