Lugha Nyingine
Bidhaa za kitamaduni zenye haki mmiliki ya ubunifu za China zawa na mvuto duniani

Watu wanatembelea maonyesho yaliyoanzishwa na Pop Mart katika Mnara wa Lulu ya Mashariki wa Shanghai, China, tarehe 3 Septemba 2026. (Xinhua/Wang Xiang)
Kampuni ya Pop Mart ya China imefungua duka lake kubwa zaidi nchini China kwenye sehemu ya makutano yenye pilika nyingi zaidi kando ya Ziwa Xihu mjini Hangzhou ambalo ni moja ya maeneo yenye uwakilishi zaidi ya kitamaduni nchini China.
Muda mrefu kabla ya milango kufunguliwa Jumamosi, umati wa watu ulikuwa tayari umetembea kwa miguu kwa kufuata njia ya kupita duka la Hubin Yintai in77 mjini Hangzhou, ili kuwahi kuangalia duka hilo jipya.
Tukio jipya linalotokea Hangzhou ni mfano mdogo wa wimbi kubwa linaloenea kote nchini China, la kuenea kwa kasi kwa uchumi wa bidhaa zenye IP (haki milikii) zinazojitokeza China.
Kwa kuunganisha utamaduni wa jadi na uchumi wa vitu vinavyopendwa, vitu hivi vyenye haki mmiliki ya ubunifu vinaendelea kuwa maarufu kote duniani.
Ripoti ya kifedha ya kampuni ya Pop Mart ya 2025 ilionyesha wimbi hilo, kuwa mfululizo wa toleo la "The Monsters", wenye mdoli maarufu wa Labubu, umekuwa ni mdoli wenye haki mmiliki ya ubunifu ya kiwango cha dunia na mapato yake yamefikia Yuan bilioni 14.16, likiwa ni ongezeko la asilimia 365.7 kwa mwaka.
Ripoti iliyotolewa na Kundi la Ushauri la Boston (BCG) mwaka huu, inaonyesha kuwa asilimia 74 ya watu waliohojiwa duniani kote walikuwa wamesikia kuhusu midoli yenye haki mmiliki ya ubunifu ya China, huku midoli ya kisasa ikifikia kiwango cha juu zaidi cha kufahamika kwa takriban asilimia 91.
Ofisa wa kampuni ya PopMart amesema, “midoli yenye haki mmiliki ya ubunifu ya China imesababisha ongezeko la matumizi duniani kwa sababu inaonyesha hisia za kitamaduni zinazowavutia watumiaji duniani kote."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



