Lugha Nyingine
Mfereji wa Pinglu utahimiza muunganiko wa kikanda na maendeleo yanayohusiana na bahari

Meli inapita kwenye Mfereji wa Pinglu karibu na kituo cha Madao. (Picha imetolewa kwa hisani ya Kampuni ya Mrefeji wa Pinglu)
Meli inayobeba makontena iitwayo Beigang Canal 001, jumatatu ilifanya usafiri wa majaribio kuelekea kwenye eneo la uendeshaji la Bandari ya Qinzhou katika Mkoa wa Guangxi, kusini mwa China. Wakati mfereji wa Pinglu unakaribia kufunguliwa, mto na bahari, ambavyo kwa muda mrefu vilitenganishwa na milima, hatimaye vitaunganishwa.
Ukiwa ni sehemu muhimu ya "Ukanda Mpya wa Kimataifa wa Biashara ya Nchi Kavu na Bahari" unaounganishwa na Mpango wa China wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na pia ni mfereji wa kwanza unaopangwa kuunganisha mto na bahari katika mpango wa jumla wa kitaifa tangu mwaka 1949, Mfereji wa Pinglu wenye urefu wa kilomita 134.2 unaweka njia fupi zaidi, yenye gharama nafuu zaidi, na rahisi zaidi ya kufikia bahari kwa eneo la kusini-magharibi mwa China. Mradi huu pia unaongeza mtandao wa mito wa China.
Ujenzi wa mfereji huo ulianza Agosti 2022. Wafanyakazi zaidi ya 20,000 kutoka makabila mbalimbali walifanya kazi pamoja huko Guangxi kwa zaidi ya siku 1,400, ambapo wakifuata mpango wa jumla wa serikali kuu, walifanya ushirikiano na watu wenyeji, kupata mafanikio makubwa ya kiteknolojia, na kuleta muunganiko wa kiviwanda.
Mfereji huo pia unaongeza njia yenye manufaa kwa pande zote kati ya watu bilioni 1.4 wa China na karibu watu milioni 700 wa nchi za ASEAN. Baada ya kukagua mfereji huo, mabalozi kutoka nchi za ASEAN, walipongeza kuwa utarahisisha mzunguko wa bidhaa, na kuimarisha uhusiano na mawasiliano kati ya watu.

Picha iliyopigwa kutoka angani ikionesha Mfereji wa Pinglu na mji wa Qinzhou, Mkoa wa Guangxi, China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



