Lugha Nyingine
Afrika Kusini yatafuta ushirikiano wa kina zaidi na China katika sayansi na uvumbuzi
Katibu Mkuu wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi ya Afrika Kusini, Mlungisi Cele, amesema Afrika Kusini inatafuta ushirikiano wa kina zaidi na China kwenye sayansi, teknolojia na uvumbuzi, kufuatia ushiriki wake katika Kongamano la 19 la Uvumbuzi la Pujiang mjini Shanghai.
Bw. Cele amesema, Afrika Kusini imeshiriki kwenye kongamano hilo kama Nchi Mgeni wa Heshima, ikiwa ni nchi ya kwanza ya Afrika kupewa hadhi hiyo, ambayo imetoa fursa kwa Afrika Kusini kuimarisha ushirikiano wa kisayansi na China.
Bw. Cele anaona, ushiriki wa Afrika Kusini kwenye kongamano hilo unatoa mchango muhimu katika kuimarisha ushiriki wake ndani ya BRICS, ushiriki wake wa kimataifa na ushirikiano kati yake na China.
Kwenye kongamano hilo, ujumbe wa Afrika Kusini pia ulihudhuria mjadala kuhusu njia za China za kuwatambua, kuwalea na kuwaunga mkono vijana wenye vipaji vya sayansi na ujasiriamali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



