Lugha Nyingine
Sudan Kusini yaanza ujumuishaji wa vikosi vya upinzani
(CRI Online) Septemba 15, 2026
Jeshi la Ulinzi la Watu wa Sudan Kusini (SSPDF) Jumatatu wiki hii liliagiza wapiganaji wote wa kundi la Agwelek wakusanyike kwenye eneo maalum katika Wilaya ya Terekeka, Jimbo la Equatoria ya Kati, na muda wa kuripoti unaanza tarehe 15, Septemba, kwa ajili ya kujumuishwa rasmi katika jeshi la serikali.
Agizo hili linaashiria hatua muhimu ya kivitendo kuelekea kutekeleza makubaliano ya amani yaliyofikiwa Januari mwaka 2022 kati ya serikali ya Sudan Kusini na kundi hilo.
Msemaji wa SSPDF, Lul Ruai Koang, amesema agizo hilo linaanza kufanya kazi Jumanne wiki hii, na linahusu vikosi vilivyopo Juba, Greater Tonj katika Jimbo la Warrap, na kaunti ya Twic East katika Jimbo la Jonglei.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



