Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini asema nchi yake itatumia uanachama wa BRICS kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema nchi yake itatumia uanachama wa BRICS kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kupanua biashara na uwekezaji na kuleta manufaa halisi kwa watu wake.
Katika taarifa iliyotolewa kufuatia Mkutano wa 18 wa Kilele wa BRICS uliofanyika huko New Delhi, India, rais Ramaphosa amesema kundi la BRICS ni jukwaa muhimu la kujenga mahusiano ya kisiasa na kiuchumi yanayonufaisha nchi hiyo na watu wake.
Rais Ramaphosa amesema, kupitia BRICS, Afrika Kusini itaendelea kuongeza sauti ya nchi za Dunia ya Kusini kwa utaratibu shirikishi wa kimataifa uliokita mizizi katika kuheshimiana na kunufaishana. Pia Afrika Kusini itaendelea kutumia uanachama wa BRICS kuendeleza uchumi wao na kuboresha maisha ya watu wao.
Rais Ramaphosa amesema zaidi ya asilimia 20 ya biashara ya Afrika Kusini inafanywa na nchi nyingine za BRICS, na inanufaika na mitaji ya maendeleo inayotolewa na Benki Mpya ya Maendeleo ya kundi hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



