Kikundi cha madaktari wa China chatoa huduma za afya bila malipo kwa wafanyakazi wa hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania.

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2026

Kikundi cha 28 cha madaktari wa China kilichopo Tanzania Bara, kinatoa dawa na vifaa tiba kwa wafanyakazi walio mstari wa mbele katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania, tarehe 12 Septemba 2026. (Picha imetolewa na Xinhua)

Kikundi cha 28 cha madaktari wa China kilichopo Tanzania Bara, kinatoa dawa na vifaa tiba kwa wafanyakazi walio mstari wa mbele katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania, tarehe 12 Septemba 2026. (Picha imetolewa na Xinhua)

Kikundi cha 28 cha madaktari wa China walioko Tanzania bara, Jumamosi kilitoa ushauri wa kimatibabu na huduma za afya bila malipo kwa wafanyakazi wa mstari wa mbele katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania.

Kikundi hicho kilitoa ushauri, upimaji wa mwili na tathmini za afya, uliofanywa na wataalamu wa ugonjwa wa moyo, upasuaji wa neva, matibabu ya maradhi ya mikono na miguu, masikio, pua na koo, na matibabu ya jadi za China.

Madaktari hao pia waligawa dawa bila malipo na kutoa vifaa tiba. Mbali na hayo, walitoa mafunzo kuhusu uamshaji wa moyo na mapafu, usalama wakati wa kazi mbugani na matibabu ya dharura kwa majeraha na magonjwa, ikiwasaidia wafanyakazi kuimarisha uwezo wao wa kulinda afya zao wanapokuwa kwenye eneo la kazi.

Mkuu msaidizi wa Jumba la Makumbusho la Mali ya Urithi wa Jiolojia la Ngorongoro-Lengai Bw. Mashaka Ramadhani, amesema wafanyakazi walio mstari wa mbele katika eneo la hifadhi, mara nyingi hufanya doria katika eneo hilo, na kujiweka katika hatari za kiafya. Wakati huo huo, upatikanaji wa huduma za afya unakuwa mgumu kwa sababu ya aina ya kazi wanayofanya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha