Lugha Nyingine
China yaelezea ufuatiliaji zaidi kuhusu hali inayoendelea kuwa mbaya Yemen, na kwenye bahari ya Sham
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Guo Jiakun, amesema China ina wasiwasi mkubwa kuhusu vifo vya raia wasio na hatia, na uharibifu wa vituo vya nishati na miundombinu mingine ya kiraia, kutokana na kuongeza kwa hali mbaya nchini Yemen na kwenye Bahari ya Sham.
Bw. Guo amesema mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia yanayoathiri maisha ya watu hayakubaliki, na machafuko yanayoendelea kuongezeka katika eneo hilo hayamnufaishi mtu yeyote, na mamlaka ya nchi na usalama wa nchi zote unapaswa kuheshimiwa.
Habari zinasema kundi la Wahouthi wa Yemen hivi karibuni lilishambulia miji minne kusini mwa Saudi Arabia, na kuwajeruhi raia zaidi ya 70 na kuharibu vituo vingi vya nishati na miundombinu mingine ya kiraia, wahouthi wamesema walishambuliwa pia na kupata vifo na majeruhi.
Bw. Guo amesema China inatoa wito kwa pande husika kujizuia, kupunguza hali ya wasiwasi kwa njia ya mazungumzo, na kufanya juhudi za kupunguza mvutano haraka iwezekanavyo. Amesema njia pekee inayofaa ya kuondoa hali wasiwasi, ni kutatua mizozo kwa njia za kisiasa na kidiplomasia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



