Lugha Nyingine
Mashindano ya Video fupi ya Guizhou Xijiu 2026 “Maisha Mazuri” yaanza rasmi

Picha kwa hisani ya waandalizi
Tarehe 9 Septemba, Mashindano ya video fupi ya Guizhou Xijiu 2026 ya “Maisha Mazuri” yenye kichwa cha“Kunywa pombe la Xijiu katika Usiku wa Katikati ya Majira ya Mpukutiko", ambayo yanaandaliwa na Guizhou Xijiu, yalizinduliwa rasmi katika Studio Namba 1 ya People's Daily Online.
Mashindano hayo yenye mada kuu ya “Maisha Mazuri” yametenga vitengo vinne vya ubunifu: mandhari nzuri, chakula kitamu, makazi mazuri na desturi nzuri. Hakuna ukomo kwa muundo wa video zinazoshiriki. Filamu za hali halisi ya maisha, filamu fupi za tamthilia, Vlog, au video za safari zote zinakaribishwa.
Mashindano hayo yanakaribisha wabunifu wote mtandaoni, na kwa mara ya kwanza yamefungua fursa ya ushiriki wa kimataifa. Washiriki wa nje ya China wanaweza kushiriki kupitia majukwaa ya TikTok na YouTube. Kazi za video zinazowekwa #MidAutumnWithXijiu au #Xijiu2026ShortVideoContest zitachukuliwa kuwa zimefanikiwa kushiriki. Kipindi cha ukusanyaji wa kazi ni kuanzia tarehe 9 Septemba 2026 hadi tarehe 10 Oktoba saa 6:00 usiku (24:00 (UTC+8)) . Kwa maelezo zaidi, unaweza kubonyeza sentensi hii ili utape mwongozo wa kushiriki.

Picha kwa hisani ya waandalizi
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



