Bw. Wang Yi asema Rais Xi ameweka dira kwa maendeleo yenye ubora wa juu ya ushirikiano mpana zaidi wa BRICS

(CRI Online) Septemba 14, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi, amesema Rais Xi Jinping wa China kuhudhuria mkutano wa kilele wa BRICS nchini India kuna umuhimu mkubwa wa kimkakati katika kuelekeza mwelekeo wa maendeleo yenye ubora wa juu wa ushirikiano mpana zaidi wa BRICS.

Bw. Wang amesema, ziara hiyo ya Rais Xi katika Asia Kusini pia imeimarisha nguvu ya umoja kati ya nchi za Kusini mwa Dunia.

Bw. Wang Yi ameyasema hayo alipokutana na wanahabari kuzungumzia ziara ya Rais Xi nchini India kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Kilele wa BRICS Jumamosi na Jumapili.

Bw. Wang Yi amebainisha kuwa ziara ya Rais Xi imetoa msukumo mpya kwenye ushirikiano wa BRICS, kuiwezesha Dunia ya Kusini, na pia kuweka dira ya uhusiano kati ya China na India.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha