Watu 26 wafariki katika ajali ya moto shuleni mashariki mwa DRC

(CRI Online) Septemba 11, 2026

Vyombo vya habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) vimeripoti kuwa, wanafunzi 26 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika ajali ya moto mkubwa uliozuka jana huko Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa nchi hiyo.

Ripoti hizo zinasema, miili ya marehemu imepelekwa hospitali za eneo hilo, na idadi kamili ya watu waliofariki bado haijajulikana, na kwamba wanafunzi wengi waliovuta moshi wanapatiwa matibabu.

Moise Lubala, ofisa wa mtaa huo, aliwaambia waandishi wa Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, zaidi ya nyumba 80 ziliharibiwa na moto huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha