Lugha Nyingine
AU yaadhimisha miaka 24 na kutoa wito wa umoja wa bara na ushawishi wa dunia
(CRI Online) Septemba 11, 2026
Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf ametoa wito wa kurejea tena ahadi ya Muungano wa Afrika, mshikamano na umoja wa bara hilo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jumatano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Afrika inayoadhimishwa Septemba 9, Bw. Youssouf amesisitiza kuwa vipaumbele vya Umoja huo vimejikita zaidi katika kuongeza kasi ya maingiliano ya kiuchumi, kuendeleza amani na usalama, na kuimarisha sauti ya Afrika kimataifa.
Pia ametoa wito kwa nchi wanachama, jamii za kiuchumi za kikanda, sekta binafsi, mashirika ya kiraia na vijana kufanya uratibu kuelekea ujenzi wa bara la Afrika lenye maingiliano, linalojiamini, na lenye uwezo kamili wa kutengeneza hatma yake lenyewe.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



