Sudan Kusini yaiaga timu ya matibabu ya China iliyomaliza muda wake

(CRI Online) Septemba 10, 2026

Serikali ya Sudan Kusini na Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini zimeiaga timu ya 13 ya madaktari wa China iliyomaliza muda wake, na kuwakabidhi wajumbe wa timu hiyo vyeti vya kutambua mchango wao na kukaribisha rasmi timu ya 14 ya madaktari wa China.

Katika hafla hiyo iliyofanyika jana mjini Juba, Waziri wa Afya wa Sudan Kusini Luke Thompson Thoan Teny amesema, timu inayoondoka ilitoa huduma za matibabu kwa jamii za huko na kutoa mafunzo kwa lengo la kuimarisha uwezo wa nguvukazi ya sekta ya afya nchini humo.

Kaimu Balozi wa China nchini Sudan Kusini Huo Ying amesema, timu ya 13 ya madaktari wa China imekumbatia moyo wa timu za madaktari wa China.

Kiongozi wa timu ya 13 ya madaktari wa China nchini Sudan Kusini Zhang Erqing amesema, ikiwa nchini humo, timu hiyo ilitoa ushauri kwa zaidi ya wagonjwa 13,500, kutibu wagonjwa 1,700 waliolazwa, kufanya upasuaji zaidi ya 200, na kuokoa wagonjwa mahututi zaidi ya 50.

Kiongozi wa timu ya 14 ya madaktari wa China nchini Sudan Kusini Zhang Jinguo ameahidi kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kutoka timu ya 13, na kufanya kazi kwa karibu na wafanyakazi wazawa kuboresha afya ya umma nchini Sudan Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha