Xi Jinping atoa salamu za Siku ya Walimu, ahimiza kuwaandaa vijana wenye uwezo kwa ajili ya ustawishaji wa taifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 10, 2026

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa salamu za pongezi kwa walimu na waelimishaji kote nchini China kabla ya Siku ya Walimu, ambayo huadhimishwa Tarehe 10 Septemba kila mwaka nchini China.

Katika salamu zake za pongezi jana Jumatano, Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito wa kuwataka walimu wa nchi nzima kuongeza weledi na uwezo wao wa kitaaluma, na kuwaandaa vijana wa kizazi kipya ili wabebe jukumu la kutimiza ustawishaji wa taifa.

"Katika muda mrefu uliopita, walimu wa nchi nzima wamejitolea katika kazi za elimu, wakitoa ujuzi na kuwaandaa vijana wenye akili zaidi," amesema Xi, na kupongeza mchango mkubwa uliotolewa na walimu kwa ajili ya mambo ya Chama na serikali.

Xi amesisitiza umuhimu wa kutekeleza jukumu la kimsingi la elimu la kuwaelimisha watu maadili, na kuwapa wanafunzi ujuzi wa kufuata maadili na mienendo ya kazi kwa vigezo vya juu.

Pia ametoa wito wa kuwaelimisha umma kuongeza heshima kwa walimu na waelimishaji, kuwatia moyo kuunga mkono elimu, na kukusanya nguvu zote za kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu katika elimu.

China imekuwa na mfumo mkubwa zaidi wa elimu duniani, kwa kuwa na shule takriban 440,000 za aina mbalimbali zenye wanafunzi milioni 280 na walimu milioni 18.7 .

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha