Lugha Nyingine
WHO yasema mlipuko wa Ebola nchini DRC unaongezeka
Ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema, mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unaendelea kuenea, huku mwelekeo wa maambukizi kwa njia mbalimbali ukionekana katika mikoa na kanda za afya.
Ripoti hiyo iliyotolewa jana jumanne, imesema mwelekeo huo unaongeza nguvu ya mlipuko wa njia tofauti, kwa kupungua kwa maambukizi katika baadhi ya sehemu, sambamba na kuongezeka na kuendelea kuenea katika maeneo mengine ya kijiografia.
Ripoti hiyo pia imesema, katika wiki ya Agosti 30 hadi Septemba 6, uwiano wa vifo vilivyothibitishwa katika jamii ulifikia asilimia 75, ikiwa ni uwiano wa juu zaidi kwa wiki kushuhudiwa wakati wa kuwasilisha ripoti, na ikiwa ni juu zaidi ya asilimia 56.6 ya wiki mbili kabla ya kipindi hicho.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



