China na Rwanda zazindua mradi wa upanuzi wa barabara mjini Kigali

(CRI Online) Septemba 09, 2026

Maofisa wa Rwanda na China wamezindua rasmi mradi wa upanuzi wa barabara na ukarabati katika mtandao wa usafiri kwenye mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Kwa mujibu wa Wizara ya Miundombinu ya nchini Rwanda, mradi huo wenye urefu wa kilomita 10 kutoka Prince House hadi Masaka mjini Kigali, ni mradi wa karibuni unaotekelezwa nchini humo kwa msaada wa China.

Waziri wa Nchi katika Wizara ya Miundombinu nchini Rwanda, Claudien Bizimungu amepongeza mradi huo akisema ni mfano mwingine wa urafiki imara na wa muda mrefu kati ya Rwanda na China.

Naye Balozi wa China nchini Rwanda Gao Wenqi amesema mradi huo ni alama ya hatua mpya ya urafiki kati ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha