Trump atoa agizo bidhaa za Canada kuondolewa kwenye orodha za kandarasi ya serikali ya Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 09, 2026

Meli ya makontena inaonekana ikiwa imemetia nanga kwenye bandari ya Vancouver, British Columbia, Canada, Agosti 25, 2026. (Picha na Liang Sen/Xinhua)

Meli ya makontena inaonekana ikiwa imemetia nanga kwenye bandari ya Vancouver, British Columbia, Canada, Agosti 25, 2026. (Picha na Liang Sen/Xinhua)

NEW YORK - Rais wa Marekani Donald Trump ametoa agizo bidhaa za Canada kuondolewa kwenye orodha za kandarasi ya serikali ya Marekani ili kukabiliana na ushuru wa kulipiza wa Canada.

"Ninaiagiza GSA (Mamlaka ya Huduma za Utawala), ikifanya kazi na USTR (Mwakilishi wa Biashara wa Marekani), kuchukua hatua zote zinazohitajika KUONDOA bidhaa zenye asili ya Canada kutoka kwenye Ratiba za Mikataba ya Ununuzi ya GSA isipokuwa pale Canada itakaporejesha usawa na haki kamili kwa Wakulima na Kampuni za Marekani," Trump ameandika katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Truth Social jana Jumanne.

"Canada hairuhusu wakulima wetu bora wa bidhaa za maziwa kuuza katika Soko la Canada, na kuwa sababu pekee inayofanya Canada kutengeneza magari ni kwa sababu ya mikataba ya awali mibaya ya biashara wakati Marais wengine walipokuwa ofisini," Trump amesema.

"Canada imekuwa ikitunyonya kwa miaka mingi. Serikali ya Canada, ikiwemo za Mikoa yake, zimepiga marufuku biashara ndogo na kampuni za Marekani kuuza katika masoko yao ya manunuzi ya serikali. Hiyo si kunufaishana kwa usawa, ni ulaghai wa biashara wa Canada." Trump amesema

"Kuanzia sasa, HAKUNA USAWA - HAKUNA RUHUSA YA KUINGIA!" Trump ametangaza.

Agizo hilo linakuja huku kukiwa na kupamba moto kwa mivutano ya kibiashara kati ya Marekani na Canada. Marekani iliweka ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa za Canada zenye thamani ya dola bilioni 20, ulioanza kutumika Agosti 22, hatua iliyosababisha Canada kulipiza kisasi kwa kuweka ushuru unaolingana na huo kwenye bidhaa za Marekani zenye thamani sawa, ambao ulianza kutumika rasmi jana Jumanne.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha