Lugha Nyingine
Uganda yateua kampuni ya Vitol kuuza mafuta ghafi
(CRI Online) Septemba 08, 2026
Uganda imeteua kampuni ya kimataifa ya nishati na bidhaa ya Vitol kuuza mafuta ghafi ya nchi hiyo kabla ya uuzaji wa mapema mwakani uliopangwa.
Kampuni ya Mafuta ya Uganda (UNOC) imesema katika taarifa yake iliyotolewa jana kwamba, kampuni ya Vitol itauza mafuta ghafi yaliyotengwa kwa serikali ya Uganda na UNOC, wakati nchi hiyo ikiingia katika awamu ya mwisho ya maendeleo ya mafuta.
Uteuzi huo unaashiria hatua muhimu kuelekea nchi hiyo kuingia katika soko la kimataifa la mafuta ghafi, huku Vitol ikitarajiwa kutumia biashara yake ya kimataifa, soko na uzoefu wake katika ugavi kuunganisha mafuta ghafi ya Uganda na wanunuzi wa kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



