Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China akutana na Waziri Mkuu wa Qatar

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Septemba 7, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani hapa Beijing China jana Jumatatu.
Waziri mkuu Li amesema, Qatar ni mshirika muhimu wa kimkakati wa China katika Mashariki ya Kati na eneo la Ghuba, China inapenda kushirikiana na Qatar katika kuongeza zaidi mawasiliano na uratibu, kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya kila upande, na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili ili kuleta manufaa makubwa zaidi kwa wananchi wao.
Li ametoa wito wa kutaka pande hizo mbili kuhusisha zaidi mikakati ya maendeleo na kuungana mkono, kusukuma mbele ushirikiano wenye sifa bora wa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuzidisha ushirikiano katika nishati ya jadi, nishati mpya, miundombinu, AI na mambo ya fedha ili kufikia ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja kwenye kiwango cha juu zaidi. Li amesema, "China inakaribisha uwekezaji wa Qatar nchini China na inaunga mkono kampuni zaidi za China kuwekeza Qatar ili kuongeza sifa bora na ufanisi wa uwekezaji wa pande mbili," na akitumai Qatar itaendelea kujenga mazingira mazuri ya maendeleo kwa kampuni za China na kuhakikisha usalama wa raia, mashirika na miradi ya China nchini Qatar.
Ameongeza kuwa pande hizo mbili zinapaswa pia kuongeza mawasiliano kati ya watu yanayohusu utamaduni, elimu, uhifadhi na utafiti wa wanyama panda ili watu wa nchi hizo mbili wawe karibu zaidi.
Amesema China inaunga mkono juhudi za suluhisho za Qatar juu ya masuala ya Mashariki ya Kati na iko tayari kushirikiana na Qatar na nchi nyingine za kanda hiyo pamoja na jumuiya ya kimataifa ili kuiwezesha kanda hiyo ijipatie amani na utulivu mapema iwezekanavyo.
Kwa upande wake Al Thani amesema Qatar inatilia maanani uhusiano wake na China, na nchi hizo mbili siku zote zinashikilia kuaminiana na kuheshimiana na zimepata matokeo ya ushirikiano wa kunufaishana na maendeleo kwa pamoja.
Amesema Qatar inapenda kushirikiana na China katika kuongeza mawasiliano kwenye ngazi zote na kuzidisha ushirikiano wa kufuata hali halisi katika uchumi na biashara, teknolojia mpya za hali ya juu na viwanda vya utengenezaji bidhaa za hali ya juu ili kukaribisha kwa pamoja muongo ujao wa dhahabu wa uhusiano wa pande mbili.
"Qatar inapongeza na kushukuru juhudi za China za kusukuma mbele amani na utulivu katika Mashariki ya Kati," Al Thani amesema, akiongeza kuwa Qatar itafanya juhudi kwa nguvu kubwa katika kutatua migogoro kwa kupitia mazungumzo na kurejesha amani katika eneo hilo.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 7, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



