Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kutaka nchi zote kusukuma mbele Mpango wa UN80
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kutaka nchi wanachama kuhimiza kazi ya kuendeleza kwa kina mageuzi chini ya Mpango wa UN80 kwenye mkutano ujao wa Baraza Kuu.
"Tunapoelekea kwenye mkutano wa 81, nazisihi nchi wanachama si tu kudumisha mwelekeo uliokuwa wa wakati wa maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, bali pia zinatakiwa kuzidisha mwelekeo huo," Guterres amesema hayo jana Alhamisi katika ripoti kuhusu mpango wa mageuzi ya mfumo wa UN kwenye Baraza Kuu, Guterres alianzisha mageuzi hayo mwezi Machi mwaka 2025, wakati ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa umeadhimisha miaka 80 ya UN.
"Miaka 80 iliyopita, watangulizi wetu walijenga Umoja wa Mataifa kwa sababu walielewa kwamba dunia yenye utatanishi ilihitaji umoja mmoja unaoweza kukabiliana na changamoto. Wajibu huo sasa ni kwetu sisi," amesema Guterres. "Kazi yetu ni kurithisha na kuendeleza Umoja wa Mataifa uwe na nguvu zaidi kuliko ule wa wakati tulipokabidhiwa, ili utakaoendeshwa kwa uratibu zaidi, wenye nidhamu zaidi katika kutumia rasilimali zake, na pia ni wenye uwezo zaidi wa kutimiza ahadi zilizotolewa kwa jina lake."Amesema kipindi cha kwanza cha mpango wa mageuzi ya UN80 ni kuhusu kuthibitisha uwezekano wa hali mbalimbali. Kipindi cha pili ni kuhusu kujaribu uwezekano huo, kujenga ushahidi, na kuamua njia. Mpango huo sasa umeingia katika kipindi cha tatu, kuhusu kutoa maamuzi na kufanya utekelezaji.
"Katika sehemu tatu za kazi ya mpango wa UN80 -- ufanisi kwenye Sekretarieti ya UN, mapitio ya utekelezaji wa majukumu, marekebisho ya muundo na miradi, mwelekeo wa maendeleo umeonekana wazi zaidi," amesema.
"Nilipoanzisha mpango wa UN80, nilizungumzia kuhusu uwajibikaji. Ninarudi kwenye neno hilo leo kwa sababu uwajibikaji ndiyo hatimaye utakaoamua kama mpango huu utafanikishwa au la," Guterres amesema.
"Kipimo halisi cha mpango wa UN80 kitakuwa miaka kadhaa baadaye juu ya uendeshaji wa umoja huo utakaokuwa tofauti kwa sababu ya machaguo ya hivi leo ya nchi wanachama, na muhimu zaidi ni kwamba, kama watu wa kote duniani wataweza au la kuona Umoja wa Mataifa utakaotoa uitikio kwa haraka zaidi, kwa ufanisi zaidi, kuchukua hatua kwa kauli moja zaidi, na utekelezaji wake utakuwa na ufanisi zaidi," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



