Lugha Nyingine
Mjumbe Maalum wa Xi ashiriki hafla ya kuapishwa kwa rais wa Zambia

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema (kulia) akikutana na Mjumbe Maalum wa Rais wa China Xi Jinping Xian Hui, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, kwenye Jumba la Jumuiya, huko Lusaka, Zambia, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Yang Guang)
LUSAKA - Mjumbe Maalum wa Rais wa China Xi Jinping Xian Hui alishiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais Hakainde Hichilema wa Zambia mjini Lusaka Jumanne wiki hii kutokana na mwaliko wa serikali ya Zambia.
Hichilema alikutana na Xian, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, kwenye Jumba la Jumuiya siku ya Jumatano.
Xian amewasilisha salamu za ukunjufu na za kutakia kila la kheri za Xi Jinping kwa Hichilema, akisema kuwa China inapenda kufanya ushirikiano na Zambia, kwa kuelekezwa na maoni muhimu ya pamoja yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, kuenzi urafiki wa jadi, kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa na kufanya ushirikiano wa kufuata hali halisi, kuungana mkono kithabiti, kuimarisha uratibu wa kimataifa, na kusukuma kwa maendeleo makubwa zaidi ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Zambia ili kunufaisha vizuri zaidi watu wa nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Hichilema amemwomba Xian kuwasilisha salamu zake za dhati kwa Xi na amemshukuru Xi kwa kutuma mjumbe maalum kushiriki kwenye hafla hiyo ya kuapishwa kwake.
Akisema kuwa Zambia inaishukuru China kwa uungaji wake mkono wa muda mrefu na wa thamani, Hichilema amesema kuwa upande wa Zambia utaendelea kufuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na kufanya juhudi za kupanua ushirikiano wa kirafiki na wa kunufaishana na China katika sekta za nishati mpya, uchumi wa kidijitali, na AI.

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema (kulia) akipeana mkono na Mjumbe Maalum wa Rais wa China Xi Jinping Xian Hui, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, kwenye hafla ya uapisho, Zambia, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Yang Guang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



