Xi atoa wito wa kuendeleza kwa kina ushirikiano kati ya China na Misri na kutoa pendekezo la Mashariki ya Kati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 03, 2026

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi na mkewe Entissar El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi na mkewe Entissar El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

CAIRO - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kutaka China na Misri kuungana mkono, kuendeleza kwa kina ushirikiano, na kuendelea kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya China na Misri yenye mustakabali wa pamoja chini ya hali ya misukosuko ya kimataifa na kikanda.

Xi ameyasema hayo jana Jumanne kwenye mazungumzo yake na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi, huku akisisitiza uungaji mkono wa China kwa nchi za kanda ya Mashariki ya Kati katika kujenga mfumo mpya wa usalama wa kanda hiyo kwa kupitia kushikilia wazo na vitendo kwa usalama wa pamoja, wa pande zote, wa kushirikiana na endelevu.

Xi ameeleza kuwa Misri ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu na Kiafrika iliyoanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1956. Amesema, viongozi wa kizazi cha zamani wa nchi hizo mbili waliwaongoza watu wao katika kufanya juhudi za kupigania uhuru wa nchi na kupinga ubeberu na ukoloni, na kuunda uhusiano wa urafiki usiovunjika.

"Katika miongo saba iliyopita, uhusiano wa China na Misri umepitia changamoto mbalimbali na kujenga uhusiano huo wenye sifa za kipekee za kuwa na usawa na kuaminiana, kuwa na urafiki na kufundishana, kuwa na mshikamano na kusaidiana, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote," amesema.

Xi amesema pande hizo mbili zinapaswa kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana, kuhusisha na kuungana mkono vizuri zaidi katika mikakati yao ya maendeleo, kutumia ipasavyo nguvu bora za ushirikiano katika sekta za jadi kama vile ujenzi wa miundombinu, nishati, kilimo na teknolojia ya mawasiliano ya habari, na kukuza mambo mapya ya ushirikiano katika nishati ya kijani, magari yanayotumia umeme, anga ya juu, uchumi wa kidijitali na teknolojia ya kilimo cha kisasa.

"Pande zetu mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano wa usalama, kupambana kwa pamoja na uhalifu wa kuvuka mipaka ya nchi, kuzidisha ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ufisadi, kuunga mkono kithabiti juhudi za kila upande za kupambana na ugaidi, na kulinda usalama wa pamoja," Xi amesema.

Kwenye mazungumzo hayo, Xi alitoa pendekezo la pointi nne kuhusu kujenga mfumo mpya wa usalama katika Mashariki ya Kati, akisema kwamba China inaunga mkono nchi za kanda hii katika kuendeleza uhusiano wa ujirani-mwema na urafiki.

Pendekezo hilo za pointi nne ni kama yafuatayo: kwanza, ili kuhimiza usalama wa pamoja wa Mashariki ya Kati, juhudi zinatakiwa kufanywa kukuza motisha za ndani za usalama wa pamoja wa kanda hii. Watu wa Mashariki ya Kati wanapaswa kuwa mabwana wa mambo yao wenyewe, ni lazima kukataa uingiliaji wa nje.

Pili, mbinu mbalimbali zinatakiwa kutumiwa kwa kusukuma mbele usalama wa pamoja katika kanda hii. Suala la Palestina bado ni kiini cha suala la Mashariki ya Kati na halipaswi kupuuzwa au kuwekwa ukingoni.

Tatu, msingi kwa usalama wa pamoja unatakiwa kuimarishwa kupitia maendeleo. Amani na utulivu katika Mashariki ya Kati inategemea kimsingi maendeleo.

Nne, uratibu wa kimataifa kwa usalama wa pamoja katika kanda hii unatakiwa kuimarishwa, na Katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa inatakiwa kufanya kazi kama kanuni za msingi kwa kushughulikia mambo ya Mashariki ya Kati.

Kwa upande wake, Rais Sisi amekaribisha ziara hiyo ya kihistoria ya Xi nchini Misri katika wakati wa maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Sisi amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano wa pande mbili siku zote umeendelea vizuri kwa utulivu, na ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata matokeo mengi mazuri.

"Misri inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na imejikita katika kusukuma mbele zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya Misri na China," Sisi ameongeza.

Amesema Misri iko tayari kuendelea kuimarisha uratibu na China ili kupunguza hali wasiwasi ya Mashariki ya Kati, kulinda utulivu wa kikanda, na kutafuta namna ya kuunda mfumo wa usalama wa kikanda.

Rais wa China Xi Jinping akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi kabla ya mazungumzo yao jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi kabla ya mazungumzo yao jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi kabla ya mazungumzo yao jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi kabla ya mazungumzo yao jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi na mkewe Entissar El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi na mkewe Entissar El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi jijini Cairo, Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha