Xi Jinping aondoka Misri baada ya ziara ya kiserikali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 03, 2026

Rais wa China Xi Jinping akiondoka Cairo baada ya ziara ya kiserikali nchini Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Xin Mengchen)

Rais wa China Xi Jinping akiondoka Cairo baada ya ziara ya kiserikali nchini Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Xin Mengchen)

CAIRO - Rais wa China Xi Jinping ameondoka Cairo jana Jumatano baada ya ziara ya kiserikali nchini Misri.

Wakati wa ziara yake hiyo, Xi alikuwa na mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi. Wakuu hao wawili wa nchi walishuhudia kwa pamoja kusainiwa nyaraka mbalimbali za ushirikiano kuhusu ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, teknolojia ya AI, uchumi na biashara, na ushirikiano wa viwanda na mnyororo wa utoaji wa bidhaa.

Nchi hizo mbili pia zimetoa taarifa ya pamoja kuhusu kuendeleza kwa kina zaidi uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

Wakiambatana na Sisi na mkewe Entissar El-Sisi, Xi na mkewe Peng Liyuan walitembelea Jumba la Makumbusho Kuu ya Misri kabla ya kuondoka nchi hiyo.

Rais wa China Xi Jinping akiondoka Cairo baada ya ziara ya kiserikali nchini Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Xin Mengchen)

Rais wa China Xi Jinping akiondoka Cairo baada ya ziara ya kiserikali nchini Misri, Septemba 2, 2026. (Xinhua/Xin Mengchen)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha