Xi asema China na Misri zimeweka mfano wa urafiki na mshikamano kati ya nchi zinazoendelea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 02, 2026

CAIRO - Rais wa China Xi Jinping amesema kwamba China na Misri zimeweka mfano wa urafiki, mshikamano na uratibu kati ya nchi zinazoendelea. Amesema, nchi hizo mbili zimekuwa na hali thabiti ya kuaminiana kisiasa, zikipata matunda mengi ya ushirikiano, na kufanya uratibu wa karibu na wenye ufanisi katika mambo ya pande nyingi.

Xi ameyasema hayo jana Jumanne katika hotuba ya maandishi aliyoitoa baada ya kuwasili Cairo kwa ziara ya kiserikali nchini Misri kutokana na mwaliko wa Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi.

Katika hotuba yake hiyo ya maandishi, Xi akiwa kwa niaba ya serikali ya China na watu wa China, alitoa salamu za dhati na za kutakia kila la kheri kwa serikali ya Misri na watu wa Misri. Amesema China na Misri zote ni nchi za ustaarabu wa kale, na zimekuwa na urafiki wa jadi ambao umedumu kwa maelfu ya miaka na kustahimili majaribu ya wakati. Xi amesema, katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, nchi hizo mbili siku zote zinaungana mkono, na kutafuta ushirikiano wa kunufaishana bila kujali hali ya kimataifa na kikanda inavyobadilika kwa namna gani.

Xi ameeleza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Marais wa nchi mbili wamehimiza kwa pamoja uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Misri kupata maendeleo ya kupiga hatua kubwa. Xi amesema, wakati wa ziara yake hiyo, atabadilishana mawazo kwa kina na rais Sisi juu ya uhusiano kati ya China na Misri, ushirikiano wa pande zote kati ya nchi hizo mbili, na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa kwa pamoja.

Amesema viongozi hao wawili pia wataandaa kwa pamoja mpango wa maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Misri, na kuandika ukurasa mpya wa urafiki kati ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha