Barabara kuu ya Serbia iliyojengwa na China yafunguliwa, kuchochea maendeleo ya kiuchumi ya Serbia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2026

Picha hii iliyopigwa Agosti 30, 2026 ikionyesha mandhari ya barabara kuu ya Ushoroba wa Danube iliyojengwa na China, Pozarevac, Serbia. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Agosti 30, 2026 ikionyesha mandhari ya barabara kuu ya Ushoroba wa Danube iliyojengwa na China, Pozarevac, Serbia. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

POZAREVAC, Serbia - Barabara kuu ya Ushoroba wa Danube iliyojengwa na China itachochea maendeleo ya kiuchumi ya Serbia, Rais wa Serbia Aleksandar Vucic amesema kwenye hafla ya ufunguzi wa barabara kuu hiyo iliyofanyika Jumapili.

Vucic, pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Serbia Sinisa Mali, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu wa Serbia Aleksandra Sofronijevic, na Zhang Zhe, kaimu balozi wa Ubalozi wa China nchini Serbia, walihudhuria hafla hiyo.

Baada ya kusafiri kwenye barabara kuu hiyo ya Ushoroba wa Danube siku hiyo ya Jumapili, Vucic alisifu sana umuhimu wake kwa maendeleo ya Serbia, akisema kwamba mradi huo utabeba jukumu muhimu katika kusukuma mbele maslahi ya kitaifa ya Serbia, kuongeza utalii wa ndani na kuchochea ukuaji wa uchumi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Barabara kuu hiyo imefunguliwa rasmi na kuanza kutumika jana Jumatatu, alitangaza Vucic.

Zhang amesema anaamini kwamba kukamilika kwa Barabara Kuu hiyo ya Ushoroba wa Danube kutavutia idadi inayoongezeka ya watalii katika maeneo ya mashariki mwa Serbia yenye mandhari nzuri.

"Hii pia inathibitisha kile tunachosema mara nyingi -- barabara huunganisha si tu miji na miji pekee, bali pia urafiki wa watu na fursa za maendeleo ya baadaye," Zhang amesema.

Kwa mujibu wa Kundi la Shandong Hi-Speed, mkandarasi wa mradi huo, barabara kuu hiyo ya Ushoroba wa Danube ni tawi muhimu la barabara kuu ya E75 barani Ulaya na mradi mwingine kinara wa ushirikiano kati ya China na Serbia.

Barabara kuu hiyo yenye urefu wa kilomita 68 ina njia nne katika kila upande mbili na imesanifiwa kupitisha vyombo vya usafiri kwa kasi ya kilomita 100 kwa saa.

Ujenzi wake ulichukua miaka mitano, ambapo katika kipindi hicho Vucic alitembelea eneo la ujenzi kwa mara saba na kuusifu mradi huo kuwa ni "barabara ya siku za baadaye."

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic akihutubia hafla ya ufunguzi wa barabara kuu ya Ushoroba wa Danube iliyojengwa na China, Pozarevac, Serbia, Agosti 30, 2026. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic akihutubia hafla ya ufunguzi wa barabara kuu ya Ushoroba wa Danube iliyojengwa na China, Pozarevac, Serbia, Agosti 30, 2026. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic akifahamishwa kuhusu barabara kuu ya Ushoroba wa Danube iliyojengwa na China, Pozarevac, Serbia, Agosti 30, 2026. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic akifahamishwa kuhusu barabara kuu ya Ushoroba wa Danube iliyojengwa na China, Pozarevac, Serbia, Agosti 30, 2026. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha