Lugha Nyingine
Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Mkuu wa Mambo ya Nje wa Syria wafanya mkutano juu ya uhusiano

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya Taher Al-Baour (kulia) akikutana na mkuu wa mambo ya nje wa Syria Asaad Hassan al-Shibani mjini Tripoli, Libya, Agosti 30, 2026. (Picha na Hazem Turkia/Xinhua)
TRIPOLILI - Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya Taher Al-Baour aliikutana na mkuu wa mambo ya nje wa Syria Asaad Hassan al-Shibani mjini Tripoli siku ya Jumapili kujadili uhusiano wa pande mbili, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya.
Kwenye mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimejadili masuala yenye maslahi ya pamoja, njia za kusukuma mbele uhusiano kati ya Libya na Syria, na namna za kuimarisha uratibu na mashauriano ya pande mbili, wizara hiyo imesema katika taarifa.
Pia wamejadili mipango kwa ajili ya kufungua tena ubalozi wa Syria mjini Tripoli, ambao ulianza tena shughuli zake siku hiyo ya Jumapili baada ya miaka 14, na unatarajiwa kuimarisha mawasiliano ya kidiplomasia na kuwezesha huduma za kibalozi, taarifa hiyo inasomeka.
Imeongeza kuwa mazungumzo hayo pia yalihusu kukamilisha taratibu za kuanzisha tena Kamati ya Pamoja ya Ngazi ya Juu Zaidi ya Libya na Syria na kusaini makubaliano ya kusimamia kazi yake, hali ambayo itafungua matarajio mapana zaidi kwa ajili ya ushirikiano katika uchumi, maendeleo, na maeneo mengine yenye maslahi ya pande zote mbili.
Baadaye siku hiyo, al-Shibani pia alikutana na Waziri Mkuu wa Libya Abdul-Hamid Dbeibah kujadili uhusiano wa pande mbili.
Ziara hiyo ya Al-Shibani ni ya kwanza kufanywa na afisa mwandamizi wa Syria nchini Libya katika miaka 14 iliyopita, kufuatia kuanguka kwa serikali ya Bashar al-Assad, wakati huu ambapo nchi zote mbili zinachukua hatua ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na usalama.
Ubalozi wa Syria mjini Tripoli ulifungwa mwaka 2012, baada ya Baraza la Mpito la Kitaifa la Libya lililokuwa likitawala wakati huo kutambua Baraza la Kitaifa la Syria la upinzani kuwa mwakilishi halali wa watu wa Syria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



