Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa "kujizuia kwa kiwango cha juu" baada ya kuanza tena kwa uhasama kati ya Marekani na Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2026

Picha hii iliyopigwa Agosti 28, 2026 ikionyesha Ikulu ya White House ikiwa nyuma ya kizuizi, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)

Picha hii iliyopigwa Agosti 28, 2026 ikionyesha Ikulu ya White House ikiwa nyuma ya kizuizi, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kujizuia kwa kiwango cha juu kufuatia kuanza tena kwa mashambulizi mwishoni mwa wiki kati ya Marekani na Iran, msemaji wake Stephane Dujarric amesema Jumatatu.

"Kuanza tena kushambuliana kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni jambo la kusikitisha sana," amesema Dujarric.

"Kwa mara nyingine tena, Katibu Mkuu anamhimiza kila mmoja kujizuia kwa kiwango cha juu. Anatoa wito wa kurejea katika shughuli ya kidiplomasia, kwenye mazungumzo ya kidiplomasia ambayo yatapelekea kupata suluhu, kusaidia kurejesha utulivu na imani katika eneo hilo," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha