Rais Xi asema China iko tayari kuzidisha ushirikiano wa washirika kimkakati wa pande zote na Misri

(CRI Online) Septemba 01, 2026

Rais Xi Jinping wa China amesema China iko tayari kuzidisha ushirikiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote na Misri, kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya nchi hizo mbili, na kuungana mkono katika kufikia mambo ya kisasa.

Kwenye makala yake iliyochapishwa na jina lake kwenye vyombo vya habari vya Misri leo Jumanne kabla ya ziara yake nchini humo, Rais Xi ametoa wito kwa China na Misri kuongeza kuaminiana na kuwa mfano katika kusukuma mbele urafiki.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kuungana mkono katika maslahi muhimu na mambo makubwa yanayofuatiliwa, na kuzidisha mabadilishano na ushirikiano katika ngazi mbalimbali na katika sekta zote.

Rais Xi pia amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kutafuta ushirikiano wa kunufaishana na wenye maslahi kwa pande zote mbili na kuweka kigezo kwa maendeleo ya pamoja.

Ameeleza kuwa China na Misri zinapaswa kujenga ushirikiano mkubwa zaidi katika mikakati ya maendeleo, kushiriki kwenye ushirikiano wenye ubora wa juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kwa hamasa kutumia kikamilifu uwezo bora na kupanua wigo wa ushirikiano wa kivitendo katika juhudi za kutoa msukumo endelevu kwenye ushirikiano wa kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha