Juhudi za Zimbabwe za kutumia magari yanayotumia umeme zapata msukumo kwa EVs za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2026

Watembeleaji wakitazama gari linalotumia umeme linaloonyeshwa kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Zimbabwe, Harare, Zimbabwe, Agosti 28, 2026. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)

Watembeleaji wakitazama gari linalotumia umeme linaloonyeshwa kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Zimbabwe, Harare, Zimbabwe, Agosti 28, 2026. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)

HARARE – Juhudi za Zimbabwe za kuongeza matumizi ya vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme zinazidi kushika kasi, huku kukiwa na shauku inayoongezeka katika magari yanayotumia umeme (EV), hali ambayo inaashiria mabadiliko kuelekea mifumo endelevu zaidi ya usafiri, kama ilivyoonyeshwa kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Zimbabwe.

Kwenye maonyesho hayo ya siku sita, ambayo yalimalizika Jumamosi katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, Idara Kuu ya Vifaa vya Mitambo ya Zimbabwe (CMED), kampuni ya serikali inayotoa huduma za usafiri na uchukuzi kwa sekta za umma na binafsi, ilivutia ufuatiliaji wa umma kwa kuonyesha magari mbalimbali yanayotumia umeme, ikiwa ni pamoja na chapa za China kama vile Nio Firefly, Geely Riddara, na magari ya kibiashara yanayotumia umeme ya King Long.

Kupitia maonyesho hayo, kampuni hiyo inalenga kutambulisha teknolojia za kijani, kujenga imani ya umma, na kuweka msingi kwa ajili ya mfumo ikolojia wa kitaifa wa vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme.

"Nia yetu si tu kutambulisha magari yanayotumia umeme bali ni kuonyesha kwamba mfumo endelevu wa vyombo vya usafiri unaweza kufanya kazi nchini Zimbabwe. Tunataka kujenga uelewa, kuwapa Wazimbabwe fursa ya kupata uzoefu wa magari ya umeme, na hatimaye kuchangia katika maendeleo ya mfumo ikolojia wa vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme," Tarisai Muzorori, afisa uhusiano wa umma wa CMED, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Kwa kutambua kwamba magari yanayotumia umeme yanabaki kuwa dhana mpya nchini humo, CMED inabadilisha mfumo wake ili kukidhi mahitaji mahsusi ya sekta hiyo wakati huohuo ikishughulikia hali ya kusita kwa watumiaji.

"Mbinu yetu ni kutambulisha magari yanayotumia umeme kulingana na mahitaji ya sekta tofauti badala ya kutumia mbinu ya saizi moja kufaa kwa wote. Hivi sasa, mfumo wetu unajumuisha magari ya abiria, na pia tunaangalia fursa za mabasi yanayotumia umeme na magari mengine ya kibiashara," Muzorori amesema.

Amebainisha kuwa kadri uelewa unavyozidi kuongezeka, gharama za chini za uendeshaji na ujumuishaji kwenye nishati mbadala vinaibuka kuwa vichocheo muhimu vya shauku, na ameongeza kuwa vizuizi kwa matumizi ya magari yanayotumia umeme ni pamoja na wasiwasi wa watumiaji kuhusu umbali wa kuendesha, uhai wa betri, muda wa kuchaji, na thamani ya kuuza tena.

Mkazi mmoja wa Harare Prestige Nota ameunga mkono wasiwasi huo, akibainisha kuwa kuanzisha miundombinu ya kuchaji na vituo vya huduma vya ndani ni muhimu kwa kujenga imani ya soko.

"Tumeona chapa za Kichina kama vile BYD zikifungua vyumba vya kuuza magari na kutoa huduma za uungaji mkono nchini Zimbabwe. Kama watu wanaweza kuhakikishiwa huduma za baada ya mauzo, labda imani katika magari yanayotumia umeme itaongezeka kadri muda unavyopita," Nota amesema.

Watembeleaji wakiangalia gari linalotumia umeme linaloonyeshwa kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Zimbabwe, Harare, Zimbabwe, Agosti 28, 2026. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)

Watembeleaji wakiangalia gari linalotumia umeme linaloonyeshwa kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Zimbabwe, Harare, Zimbabwe, Agosti 28, 2026. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha