Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa na ukosefu wa kujali kimataifa kuhusu Ebola

(CRI Online) Agosti 28, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana Alhamisi kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini New York kuhusu hali ya janga la Ebola ameeleza kusikitishwa na ukosefu wa kujali kimataifa kwa mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na ametoa wito wa dharura wa kuongeza juhudi za kuchukua hatua.

Huku akibainisha kuwa Ebola ni janga la kibinadamu linaloathiri familia na jamii kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea, Guterres amesema mlipuko huo wa sasa, ambao ni mkubwa zaidi katika historia ya DRC, unaendelea kupanuka katika eneo kubwa huku wanawake na watoto wakiathirika zaidi.

Amesema hadi kufikia tarehe 25 Agosti, watu 5,713 walikuwa wamethibitishwa kuambukizwa, kati yao 2,744 wamefariki dunia, na wagonjwa wapya takriban 500 wanaripotiwa kwa wiki.

“Kila pengo katika ufadhili na uungaji mkono wa uendeshaji shughuli linafanya mapambano dhidi ya janga kuwa na changamoto zaidi.” Gutteres amesema, akiongeza kuwa UN imetoa mpango wa kina wa mahitaji ya kibinadamu na mwitikio wenye bajeti ya dola bilioni 2.13 za Marekani, ambapo asilimia 48 kati ya hizo zinafadhiliwa.

Huku akitoa wito wa kudhibiti mlipuko huo, Guterres amesema kuwa ni muda sasa wa kuita dhamira ya pamoja ili kuchukua hatua kabla gharama haijawa ya vifo vingi zaidi, ngumu zaidi na ghali zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha