Rais wa Iran asema Marekani haitapata chochote kupitia shinikizo la kiuchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 27, 2026

Picha hii iliyopigwa Mei 1, 2026 ikionyesha mandhari ya Tehran, Iran. (Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 1, 2026 ikionyesha mandhari ya Tehran, Iran. (Xinhua)

TEHRAN - Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kwamba Marekani haitapata chochote kupitia shinikizo lake la kiuchumi dhidi ya Iran.

Ametoa kauli hiyo jana Jumatano kwenye mkutano katika mji mkuu Tehran kwa ajili ya kujadili hali ya hivi punde ya viashiria vikuu vya Iran vya sarafu, fedha za kigeni na mambo ya fedha.

Pezeshkian amesema kwamba ingawa Iran inatafuta kutatua masuala kupitia mawasiliano na mazungumzo, wakati huo huo, itasimama kidete dhidi ya shinikizo la kiuchumi, kama ilivyofanya hadi sasa.

Ameeleza imani yake kwamba Marekani haitapata chochote kupitia shinikizo lake hilo la kiuchumi katika hatua hii, akirejelea maandalizi yaliyofanywa na sekta za uchumi za utawala wake. Amesema hiyo itakuwa sawa na vita (vya siku 40), ambapo majeshi na watu wa Iran walivizuia kufikia malengo yake kwa ushujaa na uungaji wao mkono.

Mapema mwezi huu, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza "operesheni ya kiuchumi ya kuharibu zaidi kuwahi kufanywa" dhidi ya nchi yoyote inayotoa msaada muhimu kwa Iran.

Juni 18, Marekani na Iran zilitia saini nyaraka ya makubaliano (MoU) juu ya kumaliza vita hivyo kwenye eneo hilo katika pande zote, ikiwa ni pamoja na Lebanon. Chini ya MoU hiyo, zilikuwa zimepangwa kufanya mazungumzo ndani ya siku 60, ambazo zilimalizika Agosti 17, ili kufikia makubaliano ya mwisho, lakini hatma ya mazungumzo hayo bado haijulikani kufuatia kupamba moto kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili mwezi uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha