Lugha Nyingine
China yaripoti hali ya kuimarishwa kwa hatua madhubuti kwa matokeo ya kupunguza umaskini

Picha iliyopigwa Mei 15, 2026 ikionyesha mandhari ya shamba la chai katika Kijiji cha Luxi cha Wilaya ya Jingde mkoani Anhui, mashariki mwa China. (Xinhua/Zhou Mu)
BEIJING - Ripoti ya Baraza la Serikali la China imeonesha kuwa matokeo ya kupunguza umaskini nchini China yameimarishwa na kupanuliwa kwa hatua madhubuti, na wastani wa mapato ya kila mtu vijijini unaongezeka kwa utulivu.
Ripoti hiyo kuhusu kuimarishwa kwa matokeo ya kupunguza umaskini na kusukuma mbele ustawishaji wa vijiji imewasilishwa kwa kuthibitishwa kwenye mkutano unaoendelea wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, mkutano huo ambao ulifunguliwa jana Jumanne.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wastani wa mapato ya kila mtu baada ya makato mbalimbali katika vijiji vya wilaya ambazo zimeondokana na umaskini uliongezeka kutoka yuan 12,588 (dola karibu 1,855 za Marekani) mwaka 2020 hadi yuan 18,627 mwaka 2025, na kufikia wastani wa ongezeko la asilimia 8.2 kwa mwaka. Ripoti hiyo pia imeonesha hali ya kuboreshwa kidhahiri katika miundombinu ya vijijini na huduma za umma, na kupungua kwa pengo la maendeleo ikilinganishwa na maeneo mengine.
Ripoti hiyo inasema kuwa, nguvu ya viwanda ya kusaidia kuongeza nafasi za ajira imeongezwa, na juhudi zimefanywa pia ili kutuliza ajira kwa wale ambao wameondokana na umaskini. Ripoti hiyo imesema idadi ya watu wa hali hiyo wenye ajira imezidi milioni 32.
Ripoti hiyo pia imeona changamoto zinazoendelea kuwepo, ikiwa ni pamoja na hatari za kutumbukia tena kwenye hali ya umaskini kwa muda mrefu, na msingi dhaifu wa kujiendeleza katika maeneo yaliyoko nyuma kimaendeleo.
Ripoti hiyo imesema, kwa kutazama siku za baadaye, utoaji wa msaada wa kawaida utawekwa katika mkakati wa jumla wa ustawishaji wa vijiji, ambapo watu walio katika hatari ya kurudia tena kwenye hali ya umaskini na wa sehemu zilizoko nyuma kimaendeleo bado watakuwa walengwa wa kupata msaada. Imesema mkakati huo utaunganisha kazi ya uungaji mkono unaolenga kusaidia watu kujiendeleza na mfumo wa kikamilifu wa uhakikishaji wa jamii, ili kuhakikisha maisha ya kimsingi ya watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



