Botswana na kampuni ya madini inayowekezwa na China zashirikiana kuanzisha kituo cha mafunzo ya ufundi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2026

Waziri wa Elimu ya Juu wa Botswana, Prince Maele, akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano, huko Gaborone, Botswana, Agosti 24, 2026. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Waziri wa Elimu ya Juu wa Botswana, Prince Maele, akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano, huko Gaborone, Botswana, Agosti 24, 2026. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Wizara ya Elimu ya Juu ya Botswana na kampuni ya uchimbaji wa Shaba ya Khoemacau inayowekezwa na China jana Jumatatu wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuanzisha Kituo cha Ubora cha Uchimbaji wa Madini kwenye Chuo cha Ufundi cha Maun katika sehemu ya Kaskazini Magharibi ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ili kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwaandaa wafanyakazi wa kiufundi wa sekta ya madini ya nchi hiyo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo ya kutia saini iliyofanyika Gaborone, mji mkuu wa Botswana, Waziri wa Elimu ya Juu wa Botswana, Prince Maele, amesema ushirikiano huo unaonyesha "njia mpya ya kufikiria kuhusu uendelezaji wa ujuzi, elimu ya ufundi, na uhusiano wa elimu na viwanda," ili kuziba pengo la ujuzi wa kazi za viwanda.

Amesema kuwa makubaliano hayo yanalenga kuwaandaa wahitimu ambao ni "wenye ujuzi, wa kuajirika, wenye uwezo wa kufanya uvumbuzi na uwezo wa kuendana na hali mbalimbali, pamoja na uwezo wa kushiriki kwenye ushindani duniani," ili kulifanya darasa liwe karibu zaidi na mahali pa kazi, na "nadharia iweze kubadilishwa kuwa nguvu za uzalishaji."

Amesema lengo ni kuwawezesha vijana wako tayari kufanya kazi baada ya kumaliza masomo shuleni, na kuwaandaa siyo tu watafuta kazi bali pia watatuzi wa matatizo na wajasiliamali wenye ujuzi unaotumika na kuhusiana na viwanda kwa ajili ya kuingia katika kazi. Amesema kuwa "anatarajia uhusiano wenye ufanisi, ulio wa kudumu, na wa kunufaishana" utaanzishwa na mradi huo.

Chen Dexin, mkurugenzi mkuu wa Kundi la China Minmetals Corporation, kampuni mama ya Kampuni ya uchimbaji wa Shaba ya Khoemacau, ameuelezea mradi huo wa mgodi kuwa ni daraja la urafiki kati ya China na Botswana, na ameahidi kuwa kampuni hiyo itaunga mkono kwa muda mrefu maendeleo ya jamii na uchumi ya nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Kimataifa wa Botswana Phenyo Butale amesema uhusiano wa nchi hiyo na China umebadilika kuwa wa kuhamisha teknolojia badala ya kutoa msaada tu wa kifedha, jambo ambalo limeonesha mafanikio ya maendeleo ya China. Amekielezea kituo hicho kuwa ni hatua ya kuelekea kuwaandaa mafundi na wahandisi wengi wa Botswana ambao hatimaye wataongoza sekta ya madini na si tu kufanya kazi ndani yake.

Waziri wa Madini na Nishati wa Botswana Bogolo Kenewendo amesema serikali inafanya juhudi za kuandaa kigezo cha masomo ambayo msingi wake ni kazi, na kuvifanya viwanda vishiriki katika kuandaa mitalaa, akidhihirisha kuwa, ukanda wa Shaba wa Kalahari na migodi mingine ya madini ya kimsingi ni muhimu kwa kutimiza uchumi wa aina mbalimbali, ambao kwa muda mrefu unategemea zaidi almasi nchini Botswana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha