Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China atoa kanuni nne juu ya suala la Palestina

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Mfalme wa Ufalme wa Hashemite wa Jordan Abdullah II ibn Al Hussein, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 24, 2026. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu alipokuwa na mazungumzo na Mfalme wa Ufalme wa Hashemite wa Jordan Abdullah II ibn Al Hussein mjini Beijing alisisitiza kwamba kanuni nne zinapaswa kufuatwa ili kusukuma mbele utatuzi wa suala la Palestina, ambalo ni kiini cha suala la Mashariki ya Kati.
Xi amesema, kwanza, ni lazima kushikilia utatuzi wa kisiasa. Mpango wa nchi mbili ndiyo mwelekeo sahihi, ni lazima kufanya juhudi za kuanzisha tena mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israeli, ili kuanzisha nchi huru ya Palestina mapema iwezekanavyo.
Xi amesema, pili, kanuni ya "Wapalestina kutawala Palestina" inapaswa kufuatwa katika wakati wa kusukuma mbele utawala wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ujengaji upya wa Gaza baada ya vita.
Tatu, ni lazima kushikilia kanuni za ubinadamu. Jumuiya ya kimataifa, na hasa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linapaswa kubeba wajibu ipasavyo katika kulinda usalama wa raia, kuhakikisha msaada wa ubinadamu utolewe bila vizuizi, na kukomesha balaa za ubinadamu.
Nne, ni lazima kushikilia haki na usawa. Hii inamaanisha kufuata sheria za kimataifa, na kuondoa dalili na sababu za kimsingi, na pia kuchukua vitendo halisi ili suala la Palestina liweze kutatuliwa mapema iwezavyo kwa pande zote, kwa njia ya haki na ya kudumu, Xi amesema.
Kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, Xi amesema China siku zote inatetea kusimamisha mapigano kwa pande zote na kukomesha vitendo vya uadui, na kutatua migogoro kupitia njia za kisiasa na kidiplomasia, na ameongeza kuwa mamlaka ya nchi na usalama wa Jordan na nchi nyingine zote katika eneo hilo vinapaswa kuheshimiwa.
Mfalme Abdullah II amesema kuwa Jordan inasifu msimamo wa China wa kutopendelea upande wowote katika mambo ya Mashariki ya Kati na uungaji mkono wake kwa mambo ya haki ya nchi za Kiarabu, na amesema Jordan inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu na China na kuendelea kufanya juhudi za kupunguza hali wasiwasi ya mambo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



